Mbunge
wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amesema atamfikisha mahakamani Spika
wa Bunge, Job Ndugai kwa kuvunja kanuni baada ya kuwaingiza polisi
ndani ya ukumbi wa chombo hicho.
Polisi hao waliingia ndani ya ukumbi huo wiki iliyopita wakati Rais John Magufuli alipofika kwa ajili ya kuhutubia Bunge.
Kubenea
alisema kitendo cha askari kuingia ndani ya Bunge kwa mara ya mwisho
kilitokea nchini Uingereza mwaka 1930 na hakijawahi kutokea tena
isipokuwa nchini.
Alisema kuwa kesi hiyo anatarajia kuifungua Mahakama Kuu wiki ijayo kwa ajili ya kutaka tafsiri ya kanuni hiyo.
Hata
hivyo, mkurugenzi wa shughuli za Bunge, John Joel alisema hakuna
kanuni iliyovunjwa kwa askari hao kuingia ndani ya Ukumbi wa Bunge.
Wakati Kubenea akiandaa mpango huo, Kamati ya Wabunge CUF imesema Spika Ndugai ndiye chanzo cha yaliyotokea bungeni.
Ijumaa
wiki iliyopita wakati Rais akiingia kutoa hotuba ya kuzindua Bunge,
wabunge hao walipiga kelele wakitaja jina la mgombea urais wa Zanzibar
kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, kuonyesha msimamo wao
dhidi ya uamuzi wa kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa visiwa hivyo.
Walipiga
kelele hizo wakati Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein akiingia kwenye
ukumbi huo na baadaye wakati Dk Magufuli akiingia ukumbini na wakagoma
kunyamaza hadi walipotakiwa kutoka nje na askari kuitwa ndani.
Wabunge
wa upinzani wanadai kuwa Dk Shein si Rais wa Zanzibar, wala makamu
wake wa pili, Balozi Seif Ali Iddi na Spika wa Baraza la Wawakilishi,
Pandu Ameir Kificho kwa madai kuwa muda wao uliisha Novemba 2, baada ya
Uchaguzi Mkuu.
Jana wabunge wa CUF chini ya Mwenyekiti wake,
Juma Hamad Omary walitoa tamko lililokemea na kutoa tahadhari kwa mambo
mawili huku wakimtaka Ndugai kutoyumbishwa na Serikali.
Katibu
wa Umoja huo, Hamudu Hassan Bobal alisema vurugu zisingetokea endapo
Bunge hilo lingezingatia tamko la barua ya Ukawa na kusikilizwa hoja ya
mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyeomba mwongozo
akitaka kujua Dk Shein na wenzake wanaingiaje bungeni wakati madaraka
yao yaliisha tangu Novemba 2.
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip
Loading...
Home » Unlabelled » SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI KUBURUZWA MAHAKAMANI NA KUBENEA...KISA NA MKASA SOMA HAPA
Post a Comment