
WATU
wawili wakiwemo Mwanasheria na Mwalimu, wamepandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka
ya kula njama za kumuua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),
Jaji mstaafu Damian Lubuva na familia yake.
Washitakiwa hao, Mwalimu Samwel Gikaro (30) na Mwanasheria Angela Mbonde (32) walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba.
Wakili wa Serikali, Hellen Moshi
alidai kati ya Oktoba 23 na Novemba 16, mwaka huu katika maeneo tofauti
Dar es Salaam na maeneo mengine nchini, washitakiwa na wengine ambao
hawajafika mahakamani, walikula njama za kumuua Jaji Lubuva na familia
yake.
Washitakiwa
walikana mashitaka na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi
hiyo unaendelea na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.
Wakili
wa upande wa utetezi, Moses Kaluwa ambaye alifika mahakamani hapo kwa
niaba ya Wakili Peter Kibatala, aliiomba mahakama itoe dhamana kwa
washitakiwa kwa kuwa mashitaka yanayowakabili yana dhamana.
Wakili Moshi alidai Jamhuri
inatambua mashitaka hayo yana dhamana kisheria, lakini inaomba dhamana
izuiliwe kwa muda hadi watakapoona inafaa kwa sababu ya asili ya kosa,
washitakiwa hawawezi kuwa nje wakati upelelezi unaendelea.
Hata hivyo, Wakili Kaluwa alidai
sababu zilizotolewa na upande wa jamhuri hazina msingi kisheria, suala
la msingi ni mashitaka yanayowakabili kuwa na dhamana na washitakiwa
wapo tayari kutimiza masharti yatakayotolewa na mahakama.
Hakimu Simba alisema pamoja na
mashitaka hayo kuwa na dhamana kisheria, kutokana na kosa pamoja na
hatua ya upelelezi, mahakama imekubali hoja za upande wa jamhuri hivyo
washitakiwa watakuwa rumande. Kesi itatajwa tena Desemba 15, mwaka huu.
During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip. During its two year run, the project will award approximately 100 major reporting grants and provide mentoring to support the best ideas for stories on development issues. Journalists who produce the best stories published or broadcasted in media that reach African audiences, will win a major international reporting trip
Post a Comment