Loading...

Kama ni Rahisi Kununua Tuzo, Wanaosema Hivyo na Wao Wakanunue – Babutale

Babutale amezijibu shutuma za baadhi ya mashabiki nchini kuwa wasanii wa WCB wamekuwa wakinunua tuzo.

Akiongea na Prince Ramalove wa Kings FM, Tale alikuwa na maneno mafupi tu kuwajibu. “Kama ni rahisi na wao wakanunue,” alisema meneja huyo.

Jumamosi iliyopita Diamond na Harmonize walishinda tuzo za Afrimma zilizofanyika jijini Dallas, Marekani.

Alidai kuwa tuzo hizo ni za Tanzania nzima na imeonesha jinsi gani mashabiki wako nao pamoja. Amesisitiza kwa kuwaomba waendelee kuwapigia kura wasanii wote waliotajwa kwenye tuzo za MTV MAMA wakiwemo wasanii wake wa WCB, Diamond na Raymond.

Wengine ni Alikiba, Navy Kenzo, Yamoto Band na Vanessa Mdee.

Z Anto Aeleza Kwanini Amekataa ofa ya Kujiunga na WCB ya Diamond


Msanii wa muziki ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo ‘Binti kiziwi’, Z Anto amefunguka na kusema kuwa mpaka sasa kuna label zaidi ya nne ambazo zinamuhitaji kufanya naye kazi lakini amekataa kufanya nao kazi.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa yupo kimya, amesema alipata ofa ya kujiunga na WCB lakini alikataa kwa kuwa yeye mwenyewe anadai anatamani kufanya kazi nje ya WCB.

“Unajua mimi tatizo langu huwezi kufanya kazi kwa kubahatisha, mpaka saizi kuna ‘label’ nyingi zaidi ya tano zinanihitaji kufanya kazi, hivyo sipendi kukurupuka lazima nitulie nione nawezaje kujiunga na moja kati ya hizo. Maana nikibugi kuchagua ‘label’ ambayo inaweza kunisimamisha kufikia pale napotaka mimi nitakuwa nimejimaliza mwenyewe. Nilikuwa na maongezi na Babu Tale, nikapewa ofa kurekodi na kujinga WCB, lakini mimi natamani kufanya kazi nje ya Wasafi, nipo tayari kufanya kazi na Tip Top Connection” Z Anto alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EATV.

Akieleza sababu ya kukataa ofa ya kujiunga WCB, Z Anto alisema “Sisi ni washairi ujue na siku zote mafahari wawili hatuwezi kufanya kazi sehemu moja, nachoweza kuwaambia ni kwamba ukimya wangu una mambo mengi mazuri na saizi kuna label moja kubwa ambayo mimi natamani kwenda kufanya nao kazi na mambo yanakwenda sawa nitakaribia kuanza nao kazi muda si mrefu,’ alisema Z Anto

Wema Sepetu a.k.a Tanzania Sweatheart Kuolewa Hivi Karibuni


Kwa taarifa nilizozinyaka hivi karibuni hukooo Instagram ni kuwa kipenzi cha wengi ( najua wengi mtabisha) si mwingine mrembo wetu Miss TZ 2006 na CEO wa kampuni ya ENDLESS FAME the one & only WEMA ABRAHAM ISAC SEPETU anaolewa hivi karibuni na model anaekuja kwa spidi ya 4G CALISAH ABDULHAMID.

Though hawaja comfirm wenyewe kuhusiana na habari hii ila nimejiongeza tu mwenyewe baada ya kuzinyaka picha hizi...

DIAMOND PLATNUMZ NA USHER RAYMONDWAPANGA MIPANGO MIZITO

Spidi ya Diamond kulitafuta tobo la Marekani inatisha. Akiwa na collabo kibindoni na French Montana, Yo Gotti na Ne-Yo ambaye watakuwa na ziara ya pamoja Uingereza Disemba mwaka huu, muimbaji huyo wa ‘Salome’ametoa hint ya mradi mwingine ujao na role model wake mwingine – Usher.Ametoa hint hiyo Ijumaa hii wakati akimpongeza muimbaji huyo wa ‘No Limit’katika siku yake ya kuzaliwa.“Happy Birthday Bro… Can’t wait for our Big day! @usher,”ameandika kwenye Instagram.

Kwa muda mrefu Diamond amekuwa akiwataja Ne-Yo na Usher kuwa ni watu anaowaangalia sana.
Older Posts
© Copyright Swahili Tanzania | Designed By Habari Zetu Daily
Back To Top